Monday, June 6, 2016

Rais Magufuli kakutana na Balozi wa Marekani nchini, Marekani kutoa msaada ambao hauhusiani na MCC











June 06 2016 Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ambapo katika mazungumzo yao ameahidi kuwa Marekani itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.



Balozi Childress  amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo.


Tanzania na Marekani kupitia shirika letu la misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC’:-Balozi Mark Childress 


Kwa upande wake Rais Magufuli amesema serikali yake itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania.


‘Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410’


‘anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za HAPA KAZI TU zinaendelea’:-Rais Magufuli

No comments: