June 06
2016 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amekutana na waandishi wa
habari na kuzungumza mambo kadhaa ambapo kati ya hayo amezungumzia suala
la wabunge wa upinzani kusema wanaenda kwa wananchi kushtaki kutokana
na mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa Serikali ya awamu ya
tano……….
'’nataka
niseme katika jambo hili, sijajua wameshauriwa na nani japo kwenye
gazeti wamesema wameshauriwa na mshauri wao wa siasa profesa mmoja
ambaye amekuwa nje katika kipindi chote cha uhai wa mwalimu na akarudi
juzi kutoka Botswana, ndiye kawashauri kwamba hizi ndio sifa za serikali
ya kidikteta nao wakameza bila kutafakari na wanaamua kucheua bila
kuitafakari nataka niwaambie Rais ana madaraka’'
No comments:
Post a Comment